Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa dini ya kislamu kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mafunzo ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) katika kuwalea watoto katika maadili bora.
Ameyasema hayo leo baada ibada ya sala ya Ijumaa katika msikiti wa Ijumaa Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alhaj Dk.Mwinyi amesema kumekuwa na idadi kubwa ya wanawake wajane Unguja na Pemba hali ambayo inayopelekea kutelekezwa kwa watoto wengi katika jamii, hili ni moja ya tatizo kubwa katika jamii linalosababisha mmomonyoko wa maadili na kusababisha watoto wengi kuishi bila ya uangalizi wa familia.