Vijana wawili ambao ni Mohamed Said (22)na Diana Rose (20) Wakazi wa Dar es salaam wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara baada ya kukutwa na fedha takribani Tsh. Milioni 20 na simu za mkononi 27 zote zikidhaniwa kuwa ni mali za wizi zilizopatikana kwa njia ya uvunjaji wa maduka pamoja na nyumba .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amesema tukio hilo limetokea May 17,2023 katika maeneo ya Mji Mpya Wilayani Babati kufuatia doria na msako uliofanywa na Jeshi hilo ambapo wawili hao wamekamatwa wakiwa kwenye nyumba ya kulala Wageni ambapo licha ya kuwa ni Wakazi wa Dar es salaam wanadaiwa kufanya uhalifu huo Manyara.