Nchi ambazo kwa kawaida haziathiriwi na kipindupindu, sasa zimeathiriwa na idadi ya vifo imevuka ile ya kawaida ya kati ya watu 100.
Kati ya Shirika la Afya Duniani na shirika la kuhudumia watoto UNICEF, Umoja wa Mataifa unatafuta dola milioni 640 za kukabiliana na ugonjwa huo wa kuambukiza, na kuonya kuhusu “janga la kipindupindu” kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
Umoja wa Mataifa unatarajia hali kuwa mbaya, ukisema hauna rasilimali za kupambana na milipuko, na kadri inavyochukua muda mrefu
kuanza kuambana nao, ndivyo hali itakavyozidi kuwa mbaya.
“WHO inakadiria kuwa watu bilioni moja katika nchi 43 wako katika hatari ya kupata kipindupindu,” alisema Henry Gray, meneja wa matukio wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na kipindupindu duniani.
Hadi sasa mwaka huu, nchi 24 zimeripoti milipuko ya kipindupindu, ikilinganishwa na nchi 15 ilipofika katikati ya mwezi Mei mwaka jana.