Waziri wa Nishati, January Makamba leo Mei31, 2023 amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kupeleka umeme Vijijini, bado kuna takribani Vitongoji 36,101 kati ya Vitongoji 64,760 ambavyo havijafikiwa na Umeme.
“Serikali ilianza maandilizi ya zoezi la kusambaza umeme katika Vitongoji vyote 36,101 ambavyo kwa sasa havina umeme, Serikali inatambua kwamba pamoja na mafanikio ya kufikisha umeme katika kila Kijiji, bado zaidi ya 50% ya Vitongoji nchini havijafikiwa na umeme, hivyo imedhamiria kufikisha umeme katika kila Kitongiji nchini na mwaka ujao wa fedha safari hiyo itaanza kupitia utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Kusambaza Umeme katika Vitongoji (Hamlet Electrification Project – HEP).
“Kazi hii tutaifanya kwa awamu na kwa hatua lakini pia kwa utaratibu mpya ambao utaharakisha utekelezaji wa mradi”