Waziri wa Nishati, January Makamba leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake.
“Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 3,048,632,519,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake.’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #BajetiYaNishati
Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:
(i) Shilingi 2,960,702,821,000 sawa na asilimia 97.1 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,609,156,128,000 ni fedha za ndani na Shilingi 351,546,693,000 ni fedha za nje’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #BajetiYaNishati
‘Shilingi 87,929,698,000 sawa na asilimia 2.9 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi 71,637,112,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 16,292,586,000 kwa ajili ya Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #BajetiYaNishati
‘Kwa kuzingatia umuhimu wa nishati katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na burudani katika maeneo ya vijijini na vitongojini, Wizara itaendelea kuweka mkazo katika kuharakisha upatikanaji wa nishati katika maeneo hayo’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #WizaraYaNishati
‘Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC itaendelea kushiriki katika biashara ya uagizaji wa bidhaa za mafuta na kupitia kampuni yake tanzu ya TANOIL, Shirika hilo litaendelea kushiriki katika biashara ya usambazaji wa bidhaa za mafuta nchini’ – Waziri wa Nishati, January Makamba
‘Serikali pia itaendelea na ujenzi wa miundombinu ya Kuhifadhi Mafuta ya Kimkakati ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta
na kuitumia vyema jiografia yake ya kuzihudumia nchi jirani kwa biadhaa za mafuta kwa manufaa ya kiuchumi na maendeleo ya Taifa letu’ – Waziri wa Nishati, January Makamba
‘Serikali kupitia TPDC itaendelea kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Ntorya hadi Madimba mkoani Mtwara. Lengo la mradi huu ni kuongeza uzalishaji wa gesi asilia ili kukidhi mahitaji yanayoendelea kuongezeka nchini’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #BajetiYaNishati
‘Katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaanza kazi za awali za maandalizi ya mradi; kuanza tafiti mbalimbali za kitaalamu zikiwemo usanifu wa awali wa kihandisi (Pre-FEED); kuendelea kuwajengea uwezo Wataalamu wa Serikali katika uendeshaji na usimamizi”- Waziri January Makamba
(i) Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas – LNG) wa mradi; kuendelea na stadi za kisayansi na stadi za mitambo itakayosimikwa katika eneo la mradi na kufanya tathmini kuhusu hali za wananchi waliolipwa fidia ili kupisha mradi (post – compensation livelihood study). Aidha, Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa Sheria Mahsusi ya mradi huu, itakayosimamia uendeshaji na utekelezaji wa mikataba iliyoingiwa’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #BajetiYaNishati
‘Serikali katika mwaka ujao wa fedha itajenga Chuo kikubwa cha Kimataifa cha ufundi katika Gesi na Mafuta pamoja na Umeme mkoani Lindi. Pia, ili kupanua fursa na kushamirisha maendeleo ya viwanda na kuongeza ajira’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #BajetiYaNishati
‘Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi itaanzisha Eneo Maalum la Kiuchumi (Special Economic Zone) katika eneo la mradi ili kuvutia viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazonufaika na miundombinu ya kiuchumi, ikiwemo bandari na umeme wa uhakika pamoja na gesi, itakayokuwepo kutokana na utekelezaji wa mradi huu wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 42’ – Waziri wa Nishati, January Makamba #BajetiYaNishati