Waziri wa Nishati, January Makamba leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2023/2024.
Na Miongoni waliosimama kuchangia hoja ni Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Immanuel Kingu..“Na kule wanakopita watu wa CHADEMA wanapiga propaganda kwamba Rais anaweka mabango, nataka nikuambie ukiona mtu anapiga kelele jua umembana vizuri, Mama amewashika kwelikweli kupitia Wizara yako January” Elibariki Kingu, Mbunge wa Singida Magharibi.
“Nataka niwaombe Wabunge wote tuendelee kumuunga mkono January na Mama Samia na Wizara hii, tuendelee kuwashika mkono. Kazi wanayoifanya ni kubwa. Sisi kwenye Ilani tuliwatuma mtuwashie umeme, umeme unawaka unataka nisikusifie?”
“Na kule wanakopita watu wa CHADEMA wanapiga propaganda kwamba Rais anaweka mabango, nataka nikuambie ukiona mtu anapiga kelele jua umembana vizuri, Mama amewashika kwelikweli kupitia Wizara yako January”-Elibariki Kingu, Mbunge wa Singida Magharibi.