Zimbabwe itafanya uchaguzi wake wa urais na bunge tarehe 23 Agosti, Rais Emmerson Mnangagwa alisema Jumatano, wakati nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ikiendelea kupambana na mzozo wa kiuchumi unaoendelea.
Mnangagwa, aliyechaguliwa kuwa rais mwaka 2018, atakuwa anawania muhula wa pili madarakani. Kuchaguliwa kwake kulifuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa madarakani Robert Mugabe mwaka wa 2017.
Mpinzani mkuu wa mzee huyo mwenye umri wa miaka 80 ni wakili na mchungaji ni Nelson Chamisa mwenye umri wa miaka 45 ambaye anaongoza chama kipya cha Citizens Coalition for Change (CCC).
Upinzani unakishutumu chama kilicho madarakani, Zanu-PF, kwa ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa.
Siku ya Jumanne, Chamisa alimshutumu Rais Mnangagwa kwa kutokuwa wazi kuhusu tarehe za uchaguzi.
Chama cha Zanu-PF kimekuwa madarakani nchini Zimbabwe tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1980.