Leo Juni 06, 2023, Waziri wa sanaa, Utamaduni na michezo, Pindi Chana anawasilisha Bungeni Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 ya Wizara hiyo.
‘Serikali itaendelea kuziunga mkono Timu zote za Taifa zitakazofuzu kushiriki mashindano ya Kimataifa. Ili kuhakikisha hilo linatekelezwa, Serikali itaendelea kutenga bajeti ya kuhudumia Timu za Taifa kujiandaa na kushiriki Mashindano ya Kimataifa. Mfano, mwaka 2019/20 Serikali ilitenga Sh. Milioni 270 mwaka 2020/21 ilitenga Sh. Milioni 431 mwaka 2021/22 ilitenga Sh. Bilioni 1.320 mwaka 2022/23 ilitenga Sh.Bilioni 1.446 na mwaka 2023/24 Serikali imetenga Sh. Bilioni 1,066’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Kwa sasa, Wizara inaendelea na taratibu mbalimbali za Ujenzi wa Viwanja vya Mazoezi na Kupumzika Wananchi (Recreational and Sports Centres) katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma ambapo mikataba ya ujenzi imesainiwa kwa maeneo ya Dar es Salaam na Dodoma. Mkandarasi amekabidhiwa maeneo na ameanza hatua za awali za ujenzi (mobilization stage). Ujenzi wa maeneo hayo unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 54.6 na ujenzi utafanyika katika kipindi cha miezi 36.’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Serikali pia inaendelea na taratibu za ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezo katika Mkoa wa Dodoma katika eneo la Nzuguni ambapo zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa uwanja huo imetangazwa. Sambamba na ujenzi wa Uwanja wa Michezo Dodoma, pia Serikali inajiandaa kujenga Uwanja kama huo katika jiji la Arusha kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya AFCON 2027 endapo nchi za Afrika Mashariki zitashinda zabuni ya kuandaa michezo hiyo’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Serikali imeanza kukarabati miundombinu ya Michezo katika shule Teule za Michezo Nchini. Shule hizi 56 za Sekondari zinahusisha shule mbili kwa kila Mkoa, kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara ikiwa na lengo la kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali vinavyoibuliwa kutoka katika ngazi ya shule za msingi. Miundombinu ya Michezo kwenye shule zilizoteuliwa inahitaji ukarabati na ujenzi’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Katika kupambana na mbinu haramu za matumizi ya dawa za kuongeza na kusisimua misuli michezoni, Serikali kupitia Wizara ilipokea fedha dola za Marekani 21,025.06 mwezi Septemba, 2022 kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa ajili ya kuwezesha mafunzo ya kukabiliana na matumizi ya dawa na mbinu haramu michezoni’- Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
Kutokana na fedha hizo masuala yaliyofanyika ni pamoja na wajumbe 2 kutoka Tanzania walihudhuria Mkutano wa Kanda ya Tano wa Antidoping nchini Uganda mwezi Oktoba, 2022; kuwezesha kuendesha mafunzo ya Wakufunzi (ToT) kwa Maafisa 30 kutoka Wizarani, BMT, Vyama vya Michezo na Maafisa Michezo wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam; mafunzo ya uelewa kuhusu antidoping kwa viongozi 180 wa vyama vya kitaifa vya Michezo; mafunzo kwa wadau na waendeshaji wa mashindano ya michezo 100 kuhusu umuhimu wa kuwapo kwa Sheria ya antidoping; na mafunzo kwa Maafisa Michezo 38 wa mikoa, BMT na Wizara yaliyofanyika Jijini Dodoma tarehe 31 Novemba hadi 1 Desemba, 2022′ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Serikali kupitia BMT limewezesha kuzigharamia Timu za Taifa kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 Serikali kupitia BMT, imewezesha jumla ya timu 15 kushiriki katika mashindano ya kimataifa ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 3.636 kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Michezo, udhamini na harambee zimetumika’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Mafanikio mengine ni Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo Warriors) iliwezeshwa kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini Uturuki kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 10 Oktoba, 2022 ambapo timu hiyo ilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali na kushika nafasi ya saba (7) duniani. Pia, Timu hiyo ilifanikiwa kuziadhibu nchi kubwa duniani kama Japan (3-1) na Uzbekistan (3-0) na kutoka sare na nchi ya Uhispania (0-0)’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Mwaka 2022/23 Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo mpira wa miguu ambapo hivi karibuni timu zetu za Simba na Yanga zimeweza kufika katika hatua nzuri katika michezo ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Timu ya Yanga kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo ya Shirikisho imekuwa ya kwanza kufuzu kucheza fainali baada ya kuiondoa timu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa mabao 4-1 katika hatua ya nusu fainali. Aidha timu ya Simba ilifanikiwa kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka mshindi wa mabao 7-0 dhidi ya timu ya Horoya ya Guinea’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani