Ni June 6, 2023 ambapo Mbunge wa Ubungo Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ni miongoni mwa wachangiaji waliopata nafasi ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kusema kuwa nchi ya Tanzania ina utamaduni mzuri kwenye michezo kuna Simba na Yanga wanashindana na kutaniana ni jambo zuri.
“Nchi yetu kwa sasa ina utamaduni mzuri katika michezo hususan katika timu zetu mbili kubwa za Yanga na Simba, tunataniana, tunashindana na kuchekana bila kugombana. Ni utamaduni mzuri na tunakwenda vizuri” Prof. @kitilam, mbunge wa jimbo la Ubungo
#LeoBungeni
“Ni mara mbili pekee kwa nchi yetu imetokea kuwa na wizara maalum kwa ajili ya utamaduni, mara ya kwanza wakati wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere na mara pili ni mwaka jana Januari 08, 2022 pale Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia alipoamua kuunda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo”- Mhe Kitila Mbunge wa Jimbo la Ubungo
“Katika jimbo la Ubungo pekee tuna mabingwa 30 wa ngumi, kwa niaba nawapongeza kwa kazi kubwa sana. Kwa upande wa muziki pia tunampongeza Dula Makabila kwa kuchukua tuzo ya msanii bora wa kiume wa singeli “- Mhe Kitila Mbunge wa Jimbo la Ubungo
“Katika Mkoa wa Dar es Salaam hususan jimbo la Ubungo tuna mashindano ya Ndondo Cup, naomba Mhe. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo utusaidie katika viwanja vya Kinesi na TP viboreshwe kwa kuwa vinatumika katika michuano ya Ndondo Cup“- Mhe Kitila Mbunge wa Jimbo la Ubungo
“Tunaomba michuano ya Ndondo Cup iingie kwenye mfumo rasmi wa kiligi na utambuliwe, kwa kuwa michuano hii imeibua vipaji vya vijana wengi sana”– Mhe Kitila Mbunge wa Jimbo la Ubungo