Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alifunga mabao 18 na asisti 17 katika mechi 29 katika michuano yote msimu huu, lakini majeraha na hamu ya klabu hiyo kuondoa majina kadhaa ya hadhi ya juu, vinaweza kuifanya PSG kuachana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.
PSG wamemtambua Bernardo Silva kama usajili wa kipaumbele, kabla ya msimu ujao, huku uwezekano wa kuondoka kwa Neymar ukiruhusu fedha kupata huduma ya mchezaji huyo wa Manchester City.
Ripoti hiyo inapendekeza klabu hiyo itatafuta bei nzuri kwa uhamisho wa Neymar, ambaye alisajiliwa kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya Euro milioni 222 kutoka Barcelona msimu wa joto wa 2017.
Chelsea ilikabiliwa na kampeni ya kusikitisha, ikimaliza nafasi ya 12 kwenye Premier League, na meneja mpya Mauricio Pochettino anatafuta majina kadhaa ya hadhi ya juu kabla ya msimu ujao. Pochettino si mgeni kwa Neymar, baada ya kumsimamia winga huyo wakati alipokuwa meneja wa PSG msimu wa 2021-22.
Tangu kuwasili kwa Todd Boehly kama mmiliki mwenza wa klabu msimu uliopita wa joto, Chelsea wametumia zaidi ya €600m. Lakini kutokana na wachezaji kama Mason Mount na Kai Havertz kuhusishwa na uhamisho, kunaweza kuwa na nafasi ya kumsajili Neymar.