Serikali imewaagiza wananchi takribani 5000 waliyovamia na kuishi katika Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo RAZABA, kuondoka mara moja katika eneo hilo na kuikabidhi Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania TFS kulisimamia.
Agizo hilo limetolewa leo Juni 6, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa Ziara yake Eneo la Saadani na RAZABA na Mji Mkongwe Bagamoyo ya kutoa matamko ya Utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Mkoani Pwani.
Amesema maamuzi ya kuwaondoa wananchi hao yametokana na serikali kushughulikia migogoro ya ardhi ambapo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliunda timu ya Mawaziri wanane wa kisekta iliyoshirikiana na timu ya wataalam na kufika katika maeneno mbalimbali likiwemo la RAZABA na kutoa mapendekezo ambayo yaliridhiwa na baraza la Mawaziri kwa utekelezaji.
Amesema Shamba hilo lilikuwa ranchi ya Mifugo ambayo ilitolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, eneo hili lilikuwa na ukubwa wa ekari 28,097 ambazo ziligawanywa katika shamba namba 364,365/1 na 365/2 Makurunge.
“Naagiza wananchi wa eneo hili la RAZABA kuondoka mara moja kwa sababu ni mali ya serikali na kuanzia sasa lipo chini ya usimamizi wa Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania TFS,” amesema Kunenge.
Katika hatua nyingine akiwa Kijiji cha Saadani Kunenge ameagiza leseni ya kampuni ya Sea Salt kupunguza eneo la ekari 50 kati ya 2,000 zinazomilikiwa na kampuni hiyo ambalo litagawiwa kwa ajili ya wananchi wa Kajanjo.
Amemtaka Kamshna Msaidizi wa Ardhi kufuata Hati ya Mmiliki wa Sasa wa East Africa resort kwa kuwa zipo ndani ya hifadhi na hakijaendelezwa.
Amemtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Chalinze kufuta kitongoji cha Kajanjo na kuhakisha Wananchi wanahamishiwa kwenye ekari 50.
Aidha Kunenge amemuagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi, kufuta hati ya upimaji eneo la Mji Mkongwe, uliofanyika ndani ya eneo la hifadhi kwa kuwa zilitolewa ndani ya GN namba 1983 na kutatua mgogoro wa ardhi eneo la magofu ya Kaole na Familia ya Omary Sherdel