Ujumbe wa Wizara ya Maji umefanya ziara ya kutathmini maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA)
Miradi inayofanyiwa tathmini ni pamoja na mradi wa uboreshaji huduma ya maji utakaonufaisha wakazi wapatao 120,000 wa maeneo ya Kihonda,Lukobe,Mkundi, SGR na Makunganya pamoja na Mradi wa Uboreshaji huduma ya majisafi na majitaka Manispaa ya Morogoro unaofadhiliwa na serikali pamoja na shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) wenye thamani ya Tsh. Bilioni 184.
Katika ziara hiyo Wizara ya Maji imeielekeza MORUWASA kuhakikisha miradi inayoendelea kutekelezwa inakamilika kwa wakati.