Ni June 8, 2023 ambapo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA, Plasduce Mbossa amefanya mahojiano katika kituo cha Clouds Media Group kuelezea sakata linaloendelea mitandaoni juu ya Bandari ya Dar es Salaam.
‘Kuna mkataba Kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Emirates ya Dubai ambao unahusu masuala ya Bandari. Hilo ndio kubwa na la kwanza. Na mkataba huu unahusu Mashirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo Mafunzo katika masuala ya Bandari. Ushirikiano katika masuala ya TEHAMA lakini pia ushirikiano katika masuala ya uendelezaji na uendeshaji wa bandari”- Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA
Mkataba unaitwa Inter-governmental Agreement kwenye hizi Serikali mbili ukilenga katika hayo Mashirikiano niliyoyataja”
“Mkataba huu pamoja na mambo mengine unaelekeza kwamba kama tunataka kushirikiana ni lazima tukubaline katika mikataba mingine ya tofauti na huu. Kwa kawaida utekelezaji wa shughuli za bandari haufanywi moja kwa moja na Serikali Kuu lakini imekasimu kwa Taasisi kwa upande wetu ni TPA na kwa wenzetu ni DP WORLD. Ndio maana kuna kutajwa kwa TPA na DP WORLD”- Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA
‘Mkataba huu moja Kati ya masharti yake unatakiwa kuridhiwa ni Mkataba wa nchi na nchi. Ni mkataba wa Kimataifa. Ili uweze kutumika unatakiwa unatakiwa kuridhiwa na pande zote mbili. Utaratibu wetu wa kuridhia kama nchi no utaratibu ambao unatolewa na Katiba ibara ya 63, ibara ndogo ya 3E. Ambapo unataka kwamba mkataba Wenye masharti ya kuridhiwa ni lazima ipeleke bungeni kwa ajili ya kuridhiwa”- Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA
“Mkataba huu haujasainiwa wala haujajadiliwa. Kilichopo kwa sasa ni majadiliano na Serikali ikasaini mkataba huo. Na pia kwa kuzingatia sheria”– Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA
“Kuhusu DP WORLD, tuliona umuhimu wa kuongea nao kwa sababu mbali mbali, moja wapo ni kwamba sehemu kubwa ya mizigo inayokuja kwetu inatoka Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali na ukanda wa bahari ya Hindi, na mizigo yao mingi kutoka maeneo hayo inakuja kwenye bandari zetu za Afrika Mashariki hivyo tukaona kuna haja ya kuungana nao” – Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA
“Kwa kawaida meli zinapofika bandarini zinapaswa kuhudumiwa kwa haraka ili ziondoke, meli zinavyotembea ndio zinatengeneza fedha. Wenye meli hawataki meli zao zikutane na usumbufu mkubwa pindi zinaposhusha mizigo” Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)”– Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA