Ni June 8, 2023 ambapo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA, Plasduce Mbossa amefanya mahojiano katika kituo cha Clouds Media Group kuelezea sakata linaloendelea mitandaoni juu ya Bandari ya Dar es Salaam.
“Mkataba huu [wa awali] ukisharidhiwa maana yake kuna taratibu za kisheria inabidi zifuatwe za kuingia mikataba ya utekelezaji ikiwemo majadiliano. Hizo taratibu zote inabidi zifanywe ndani ya miezi 12″- Plasduce Mbossa- Mkurugenzi TPA
Kwenye mikataba ya utekelezaji tutajadili “terms” na “consideration” za pande zote mbili lakini pia na suala la muda wa mikataba ya utekelezaji.”-Plasduce Mbossa- Mkurugenzi TPA
“Hoja ya kusema kwanini mchakato huu hauhusishi Bandari ya Zanzibar ni kwa sababu TPA inahusika na upande wa Tanzania Bara. Kule nako kuna wanaohusika na Zanzibar, japo wote tupo kwenye Jamhuri moja ya Muungano wa Tanzania.”-Plasduce Mbossa-Mkurugenzi TPA
‘Serikali ina malengo mazuri ya kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinakua kwa kasi zaidi. Lakini pia naishukuru serikali kwa sababu kuna uwazi ambao unaweza tusababishia [hata] tukataa. Si kila nchi inaweza ikaenjoy hiki ambacho tunaenjoy kwamba kuna uwazi kama huu wa kuweza kujua kwamba kuna vitu gani vinaendelea.”-Plasduce Mbossa-Mlurugenzi TPA
“Serikali haijasaini mkataba wa miaka 100. Serikali haijaiuza Bandari. Serikali ina malengo mazuri na Bandari. Na sisi TPA tunahakikisha kwamba tunaendeleza malengo mazuri ya shughuli za bandari kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Na sisi kama TPA tupo committed kuhakikisha kwamba tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuwapa nafuu Watanzania ambao wanatumia Bandari zetu na nchi nyingine. Lakini pia niwaombe tushirikiane katika kuhakikisha tunaendeleza hizi shughuli za Bandari na ziwe na manufaa makubwa kwa uchumi” -Plasduce Mbossa-Mlurugenzi TPA.