Ni June 8, 2023 ambapo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA, Plasduce Mbossa amefanya mahojiano katika kituo cha Clouds Media Group kuelezea sakata linaloendelea mitandaoni juu ya Bandari ya Dar es Salaam.
“Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) itaendelea kuendesha maeneo mengine kulingana na makubaliano tutakayokuwa nayo. Lengo ni kuhakikisha kuna ufanisi na kukua kwa shughuli zingine za kiuchumi” Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari