Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mhe.Regine Hess Balozi anayeiwakilisha Ujerumani nchini Tanzania ambaye anamaliza muda wake wa utumishi nchini.
Katika mazungumzo yao yamegusia ushirikiano uliopo katika sekta afya, maji, michezo, ulinzi, uwekezaji na utalii kati ya Ujerumani na Zanzibar.
Aidha, Balozi Hess ampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuunda kamati ya maridhiano kitaifa kati ya Chama cha CCM na ACT Wazalendo.
Balozi Hess amemtambulisha Balozi mdogo wa Ujerumani atakayefanya kazi zake Zanzibar Dk. Jenny Bouraima kwa Rais Dk.Mwinyi.