Uhamisho wa kiungo Mfaransa aliyeshinda Kombe la Dunia N’Golo Kante kwenda Al-Ittihad ya Saudi Arabia unatatizwa na masuala ya afya, chanzo cha klabu kiliambia AFP siku ya Alhamisi.
Kante, 32, ana historia ya majeraha na alikosa miezi sita ya msimu wa Ligi Kuu ya Chelsea kutokana na tatizo la misuli ya paja.
Chanzo cha Al-Ittihad kilisema Kante alitia saini makubaliano ya lazima lakini klabu hiyo inachunguza matokeo ya vipimo vya afya kabla ya kukubaliana mkataba wa mwisho.
Siku ya Jumanne, klabu hiyo yenye makao yake mjini Jeddah ilimtambulisha rasmi mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or ya Ufaransa Karim Benzema mwenye umri wa miaka 35 kama mchezaji mkubwa zaidi katika historia yao.
“Kante alisaini makubaliano ya lazima, sio mkataba wa mwisho,” chanzo kilisema.
“Bado tunapitia matokeo ya uchunguzi wa afya. Ana historia ndefu ya majeraha na tunataka kuwa makini kabla ya kusaini mkataba mkubwa.”