atukio ya kuhuzunisha katika kituo hicho cha Al-Mayqoma yaligonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwezi uliopita, wakati mapigano makali baina ya jeshi rasmi la serikali na wanamgambo wa RSF yalipokuwa yakirindima katika eneo linalokizunguka kituo hicho cha watoto yatima.
Takribani watoto yatima 300 walionaswa katika mapigano makali katika mji mkuu wa Sudan wameokolewa katika tukio la kuthubutu na hatari la kuhamishwa na wahudumu wa kibinadamu.
Uhamisho huo ulitekelezwa baada ya vifo vya watoto 67 katika kituo cha watoto yatima cha Mygoma mjini Khartoum.
Walikufa kwa njaa, upungufu wa maji mwilini na maambukizi kwani mapigano yalizuia wafanyakazi kufika kwenye kituo cha watoto yatima.
Khartoum imekumbwa na mashambulizi ya anga ya kila siku na mapigano makali kati ya vikosi vinavyohasimiana tangu tarehe 15 Aprili.
Nyumba ya watoto yatima iko katika eneo ambalo limekuwa kitovu cha mapigano kati ya wanajeshi na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF).
Katika operesheni hatari, watoto 297, kama 200 kati yao walio chini ya umri wa miaka miwili walichukuliwa kwa njia ya barabara hadi usalama wa Wad Madani, kusini mwa Sudan.
Watoto wengine 95, wote kutoka kituo cha watoto yatima cha Mygoma na vituo vingine vidogo katika mji mkuu, walihamishwa mwishoni mwa wiki na kundi la wanaharakati wa ndani.