Mkataba unaokuja wa Lionel Messi na Inter Miami umezua msisimko miongoni mwa mashabiki wa nyota huyo wa kandanda wa Argentina, wakifanya idadi kubwa ya maongezeko ya watu kwenye mitandao ya kijamii na mauzo ya tiketi yakiongezeka.
Wakati Messi bado haja tumia kalamu yake kukamilisha uhamisho wake, wafuasi wa Inter Miami kwenye Instagram waliongezeka mara nne tangu mshindi huyo wa Kombe la Dunia alipofichua Jumatano kwamba ataelekea katika klabu ya Ligi Kuu ya Soka baada ya kuondoka Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
Akaunti ya Inter ilikuwa na takriban wafuasi 900,000 kabla ya Jumatano,chini ya saa 24 baada ya habari hiyo kusambaa, idadi hiyo ilikuwa imefikia wafuasi milioni 5.7.
Sasa ina wafuasi zaidi ya milioni 7.5 kwenye majukwaa yote ya kijamii na iliongeza zaidi ya wafuasi wapya milioni tano siku ya tangazo.
Kampuni ya teknolojia ya tiketi ya Logitix ilichambua mahitaji ya tiketi katika ligi nzima ndani ya saa 24 tangu Messi atangaze na kugundua kulikuwa na mara nne ya idadi ya tiketi zilizouzwa kwenye soko la kati kwa mechi za Inter Miami ikilinganishwa na kipindi chote cha mauzo cha siku 169 zilizopita. .
Bei ya wastani ya mechi za nyumbani za Inter Miami iliongezeka kutoka $31 hadi $152 huku kwa michezo ya ugenini iliongezeka kutoka $94 hadi $207, kampuni hiyo iligundua.