Ni June 9, 2023 ambapo muda huu Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga anafunguka live kupitia kipindi cha PowerBreakFast.
hapa nimekusogezea miongoni mwa nukuu zake zifahamu pamoja na kuhusu Vijana walionufaika na fursa aliyoitoa aliyoipa jina la Mchongo wa Big Joe.
“Kwenye mchongo unaokuja huu nia kubwa ni kuhakikisha kwamba tuna- connect Kati ya wafanyabiashara wakubwa wa nje ya nchi wakutane na wafanyabiashara wa Tanzania. Wakati mwingine mtu anaweza akawa ana products hajui pa kuiuza inaoza. Nina vijana wengi ambao wamefika mbali na platform ambazo zinaunganisha masoko na tumewasimamia na wapo katika hatua za mwisho, wanalima nyanya na tumeona nyanya zikioza mashambani kwa kukosa soko”- Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
“Kusingekuwa na ushindani kwenye media level, productivity isingekuwa kubwa. Clouds Media imekuwa namba Moja kwa miaka yote mpaka leo miaka 24. Lakini sasa hivi mnavuta soksi zaidi kwa sababu kuna ushindani. Huwezi kukataa kwamba ushindani haupo kwenye Media. Mtu yoyote anayekuja kufanya biashara naye vilevile anajitayarisha. Sehemu yangu ni kukaa kuangalia watoto wangu wanafanya nini? Wakihitaji msaada nawasaidia” – Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
“Kujenga nchi ni kitu muhimu sana. Kwanini nchi watu wawe maskini? Hicho kitu kila siku nakataa why? Tunahakikisha tunatoa nafasi na watu wengine wanasaidia kutoa hizo ajira. Mchongo wa Kwanza wa Big Joe wa 2021 ulikuwa na mafanikio sana”- Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
“Nafurahi kuona kupitia #MchongowaBIGJOE kuna vijana wawili tayari ni mabilionea, walinifuata kuniuliza wanipe nini kama zawadi ya shukrani, nikawaambia wasinipe chochote, wawasaidie vijana wengine kufikia malengo yao! Mwaka huu mchongo utakuwa mchongo kubwa zaidi.” -Mkurugenzi CloudsMedia- Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga