Ni June 9, 2023 ambapo CRDB Benki imekabidhi Jumla ya gawio la Shilingi bilioni 45.8 kwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ikiwa ni gawio kwa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake kutokana na uwekezaji ndani ya Benki yetu.
Mwaka huu wametoa jumla ya gawio la Shilingi bilioni 117.5 kwa Wanahisa wao baada ya kupata faida ya shilingi bilioni 351.4 baada ya kodi mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la 31% kulinganisha na faida ya shilingi bilioni 268.2 mwaka 2021.
‘Tutapunguza ile mikopo isiyolipika kwa package tutakayoiweka katika Mwaka wa Fedha unaokuja ambapo Mheshimiwa Rais analengo la kuhakikisha sekta binafsi inapendeza”- Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
‘Moja ya Sababu kwa kufanikiwa huku matokeo ya Benki Kuu kutenga Trilioni moja kwaajili ya kuzikopesha benki ili nazo ziweze kuwakopesha wadau kwa gharama ndogo na mbali na hili lillotengwa na Benki Kuu pia Mheshimiwa Rais anakuja na Package nyingine kabambe ambayo itawezesha sekta hi za benki ambazo wanazitoa Mikopo”- Waziri Mwigulu