Baada ya hivi karibuni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uzalishaji na uuzaji wa Maziwa ‘Asas’, Ahmed Asas kufunguka kuhusu kuelekea kwa kampen ya uhamasishaji kuhusu juu ya utoaji wa Elimu visiwani Zanzibar.
Sasa imeshaanza rasmi na hizi ni baadhi ya picha za matukio mbalimbali kutokea visiwani Zanzibar.
Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV alisema..’Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa watanzania kwa kutuwezesha Asas Daires kuwa namba moja katika mashindano ya maziwa kati ya makampuni yote Tanzania ambapo wiki iiliyopita kwenye maadhimisho ya wiki ya Maziwa kule Tabora tunapata faraja sana ya kuendelea kujituma na kuongeza ubunifu kila siku’- Ahmed Asas
‘Mnamo June 17, 2023 hitimisho la kampeni yetu itafanya Katika Viwanja vya Kisonge kuanzia saa kumi na mbili alfajiri ambapo kutakuwa na mambo yafuatayo yakiwemo Mazoezi ya kukimbia, Maonesho ya bidhaa za Maziwa, Burudani na Michezo pamoja na Elimu juu ya unywaji wa maziwa’- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas, Bw Ahmed Asas
‘Bila kusahau tutakuwa na mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, sisi kama Asas tunaomba wadau na wananchi wote waendelee kukaa na platform zetu tutakuwa tunaendelea kuwahabarisha kwa kile kilichosahihi hakika maziwa ni Afya’- Ahmed Asas