Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege ya Precision Air, Michael Ngaleku Shirima (80) amefariki dunia jana saa tatu usiku Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu tangu juzi June 8.
Taarifa iliyotolewa na Precision Air leo asubuhi imethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema taarifa zaidi za mazishi ya Mzee Shirima aliyefariki akiwa na umri wa miaka 80 zitatolewa na familia yake.
Kwa mujibu wa wikipedia, Mzee Michael Ngaleku Shirima alianzisha Shirika hilo la Ndege miaka thelathini iliyopita (1993) Arusha akiwa na Ndege ya Abiria watano ya Piper Aztec akisafirisha Watalii kwenda Mbuga za wanyama kama Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar ambapo miaka kumi baadae ( 2003) Kenya Airways lilinunua hisa za Shirika hilo na kupata umiliki wa 49% kwa pesa taslimu ambazo ni dola milioni mbili za Marekani.
AyoTV na millardayo.com zinatoa pole kwa Precision Air, Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa msiba huu.