Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa leo June 10,2023 amewasilisha Bungeni maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari Tanzania ambapo amesema manufaa ambayo yanatarajiwa kupatikana iwapo Bunge litaridhia azimio hilo ni pamoja na Kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka saa 24.
“Naomba pia kuchukua fursa hii kuelezea manufaa ambayo yanatarajiwa kupatikana iwapo Bunge letu Tukufu litaridhia Azimio hili na kuwezesha Serikali kuendelea na hatua zinazofuata za majadiliano na Serikali ya Dubai, baadhi ya manufaa yatakayopatikana ni pamoja na Kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24, hii itapunguza gharama za utumiaji wa Bandari yetu na itaongeza idadi ya meli zitazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 mpaka kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33”
“Kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka siku 4.5 mpaka siku 2, kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 kutokana na uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA, kupunguza gharama ya usafirishaji wa mizigo kutoka nchi za nje kwenda nchi za Jirani, kwa mfano kutoka US$ 12,000 mpaka kati ya US$6,000 na US$7,000 kwa kasha linalokwenda nchi ya Malawi, Zambia au DRC, hii italeta Watumiaji wengi kwenye Bandari ya Dar es Salaam”
“Manufaa yanayotarajiwa: kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24. Hii itapunguza gharama za utumiaji wa Bandari yetu. Matokeo yake itaongeza idadi ya meli zitakazokuja bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 mpaka kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33.“Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa.