Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makale Mbarawa, amesema iwapo Bunge la Tanzania litaridhia Azimio hilo na kuwezesha Serikali kuendelea na hatua zinazofuata za majadiliano na Serikali ya Dubai, hihi ndizo baadhi ya manufaa yatakayopatikana’
“Uwepo wa ajira za Watanzania hususan watumishi wa bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao nchi itaufanya. Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma. Vile vile Mkataba huu umeweka bayana sharti kwa Kampuni ya DP World kutumia Wakandarasi wa ndani katika manunuzi ya huduma na bidhaa pamoja na kusaidia Vyuo vya mafunzo vya Tanzania katika masuala ya elimu ya usafirishaji majini.”Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa.