Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Utoaji wa Mitaji na Uwezeshaji la UN – CDF limesema litaendelea kufadhili Vijana wa Kitanzania ambao wanabuni makampuni na Mifumo ya Kiteknolojia.
Ahadi hiyo imetolewa katika hitimisho la mafunzo kwa Vijana Wabunifu ambao walibuni makampuni zaidi ya 15 ya Kibiashara na Kifedha kwa njia ya teknolojia ambayo tayari wameonesha uwezo katika uendeshaji wake.
Aidha kampuni kama Safari Tech ambayo ilikuwa inasapoti Program ya Pesa Tech yenyewe imeweza kuwasifu kwa kazi nzuri huku wenyewe Safari Tech wakitoa mafunzo kwa vijana katika masuala mazima ya Utalii.
“Kumekuwa na faida kubwa japo wengi wanaamini ni jambo la Wazungu kumbe sio kweli inawezekana kwa wote hata Watanzania tunaweza,”.
“Tunaomba Watanzania wajitoe sana katika masuala mazima ya Teknolojia kwani kwa sasa fursa nyingi za Biashara zinapatikana huko na hata kuendelea kubuni Makampuni kwa mifumo ya Teknolojia kwani ni njia nzuri ya kujiongezea kipato,”.Amesema Iddi John ambaye ni Mwakilishi wa Safari Tech.