Mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee amechangia maelezo ya serikali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari Tanzania ambapo amesema manufaa ambayo yanatarajiwa kupatikana iwapo Bunge litaridhia azimio hilo ni pamoja na kuongezeka kwa Mapato ya Serikali.