Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema sera ya afya na Elimu bure Zanzibar itaendelea kutekelezwa kupitia ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2020-2025.
Ameyasema hayo leo tarehe 11 Juni 2023 ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akizungumza na Viongozi wa CCM ngazi ya Shina, Wajumbe wa Halmashauri Jimbo, Wilaya na Mkoa.