Fetty Wap weekend hii aliagizwa kukabidhi rekodi zake za DNA na benki baada ya kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani kwa uhusika wake katika matumizi ya dawa za kulevya katika kisiwa cha Long Island, NY.
Kulingana na TMZ, atahitajika kukabidhi rekodi zake za benki na hati za kodi pindi atakapoachiliwa kutoka gerezani, kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na Idara ya Marekebisho ya Marekani.
Zaidi ya hayo, hataruhusiwa kufungua akaunti zozote mpya za benki bila idhini ya hapo awali, na atalazimika kuwasilisha aina yoyote ya utafutaji na ukamataji wa kila kitu anachomiliki kuanzia nyumba zake hadi magari yake ikiwa atabainika kukiuka chochote.
Mbali na vikwazo dhidi yake, Fetty Wap pia atahitajika kuwasilisha sampuli ya DNA kwa afisa wake wa majaribio mara tu atakapoachiliwa kutoka gerezani na DNA hii itaingia kwenye CODIS (Composite DNA Index System) kujua hali yake juu ya matumizi ya madawa.
Mwezi uliopita, Fetty Wap alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa tukio lake la kusaidia kuendesha mtandao wa dawa za kulevya nje ya Kisiwa cha Long.
Rapa huyo wa “Trap Queen” (jina halisi Willie Junior Maxwell II) amekuwa rumande tangu Agosti mwaka jana wakati dhamana yake ilipofutwa kufuatia madai kwamba alionyesha bunduki na kutishia kumuua mtu alipokuwa kwenye simu ‘FaceTime’.