Serikali ya Rwanda na Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) Jumamosi walihitimisha makubaliano ya kuanzisha makao makuu ya Wakala wa kwanza wa Dawa barani Afrika mjini Kigali.
Mnamo Juni 10, Rwanda ilitia saini makubaliano na Umoja wa Afrika kuandaa makao makuu ya Shirika la Madawa la Afrika mjini Kigali.
Utiaji saini huo unakuja siku chache baada ya mamlaka ya Rwanda kukubali rasmi kuwa mwenyeji wa makao makuu ya AMA katika eneo lao.
Mnamo mwaka wa 2019, nchi za Kiafrika zilipitisha mkataba wa kuanzisha Wakala, ambao ulianza kutumika mnamo 2021.
Kuundwa kwake ni sehemu ya mkakati wa Umoja wa Afrika kupunguza utegemezi wa bara hilo kwa bidhaa za dawa zinazotolewa na mataifa ya kigeni.
Afrika inaagiza kutoka nje 97% ya bidhaa za dawa inazohitaji.
Shirika hilo linapaswa kudhibiti na kuoanisha soko hili katika bara la Afrika, kuhimiza uzalishaji barani Afrika na kupambana na ulanguzi wa dawa ghushi.
Kwa Minata Samaté Cessouma, Kamishna wa Afya wa AU, Afrika lazima ijitayarishe kwa magonjwa mengine ya milipuko baada ya Covid-19, na lengo la wakala litakuwa kupendekeza “suluhisho za Kiafrika”.
Zaidi ya miaka minne baada ya kupitishwa mwaka 2019 kwa makubaliano ya kuanzisha Shirika la Madawa la Afrika, hii ni hatua ya kwanza kuelekea kufanya chombo hiki kipya cha Umoja wa Afrika kufanya kazi, kulingana na Waziri wa Afya wa Rwanda, Sabin Nsanzimana.
Uajiri wa wafanyikazi utajadiliwa katika muda wa siku kumi, tena huko Kigali, wakati wa kikao cha pili kisicho cha kawaida cha Mataifa 23 ambayo yameidhinisha mkataba wa kuanzisha wakala.