Ni June 13, 2023 ambapo Dr Willibrod Peter Slaa amekutana na Vyombo vya habari kuzungumza ikiwemo ishu inayoendelea mitandaoni juu ya Bandari.
Slaa, ambaye aliwahi kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, amefafanua kuwa MOU au “Memorandum of Understanding” ni “makubaliano ya awali” ambayo pande mbili zinazotaka kuingia kwenye mkataba na kwa kawaida Serikali moja na nyingine zinatia saini.
“Nikirejea kwenye suala la MOU na “ Intergovernmental Agreement” hili si jambo geni nchini Tanzania, MOU hufuatiwa na mkataba unaoitwa Intergovernmental Agreement au kwa kifupi IGA. Hivyo mkataba huu si wa kwanza kwa Serikali ya Tanzania.”
Alieleza kuwa Tanzania imesaini maelfu ya mikataba ya uwekezaji kati yake na mataifa mengine.
Alitoa mfano kuwa Tanzania imesaini jumla ya mikataba 2,829 ya uwekezaji, yaani “Bilateral Investment Treaties (BITS)”, na nchi za kigeni mbalimbali.
Kati ya mikataba hiyo ya BITS, jumla ya mikataba 2,219 inaendelea kutumika hadi sasa.
Jumla ya mikataba yenye maslahi ya kibiashara ni 435 na ambayo inatumika ni 264.