Katibu Mtendaji BASATA Dkt Kedmom Mapana leo tarehe 13 Juni, 2023 amebainisha kuwa Baraza limedhamiria kusimamia katika Uwezeshi wa shughuli za sanaa badala ya Udhibiti ili Kuboresha ustawi endelevu wa sekta hiyo.
Ameyasema hayo wakati anaongea na Waandishi wa habari Ofisini kwake katika mkutano uliolenga kuelezea vipaumbele vya Baraza kwenye Utekelezaji wa shughuli zake Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 ikiwa ni sehemu ya ushirikishaji wadau waweze kufahamu dhamira ya kuendeleza Sanaa nchini.
Ameendelea kusema kuwa Uwezeshaji huo utaambatana kuanzisha, kuendeleza na kuratibu program mbalimbali ikiwemo mradi wa “BASATA Vibes” wakishirikiana na Ubalozi wa Ufaransa itakayozinduliwa mwezi Julai Mwaka huu ikifuatiwa na matamasha zaidi ya 20 chini vatakayotoa fursa kwa wasanii wetu kunufaika na malipo ya kazi zao katika kila tamasha.
Ameongeza kuwa, huu ni Mwaka wa pili Serikali inaendesha tamasha la Tuzo (TMA) hivyo anawakaribisha wadau ambao wapo tayari kufanya maboresho ya kusimamia na kuendesha tuzo hizo ili kupunguza kadhia.