Kamanda mkuu na rais wa zamani, anayeshutumiwa kwa kutojali baadhi ya siri nyeti za nchi na kuzuia mamlaka wakati wakijaribu kurejesha nyaraka muhimu, alikana mashtaka 37. Lakini aliichukulia siku hiyo kama tukio la kampeni, hata kama anakabiliwa na vitisho vikali kwa malengo yake ya kisiasa na uhuru wake.
Licha ya uzito wa mashtaka, Trump, alitaka kuongeza manufaa yake ya kisiasa.
Mgombea huyo wa urais wa 2024 akiwahimiza wafuasi kujitokeza katika mahakama ya shirikisho na mamia walikuja
kama alivyofanya baada ya kufikishwa mahakamani huko New York, Trump alipanga hotuba baadaye kutoka kwa moja ya vilabu vyake vya gofu na alizungumza Jumanne usiku huko, New Jersey, ambapo huwa anatumia majira ya joto.
Katika hotuba yake , Trump alikasirika na kurudia madai yake kwamba uchunguzi huo ni wa kisiasa, akawaita waendesha mashtaka “majambazi” na kudai alikuwa na shughuli nyingi kiasi kwamba hakuwa na muda wa kupitia masanduku yote ya nyaraka na kumbukumbu alizohifadhi.
Pia alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais mwaka ujao, atamteua mwendesha mashtaka maalum kumchunguza Rais Joe Biden na familia yake.
Kesi inayomhusu Trump ilifunika habari nyingi siku ya Jumanne huku wapinzani wake wa urais wa GOP kwa kiasi kikubwa walikaa mbali na hafla zozote za kampeni zao.
Mgombea mmoja wa chama cha Republican, Vivek Ramaswamy, alitaka kufaidika na tamasha hilo kwa kufika nje ya mahakama kuwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa akiwahimiza wagombea wengine wa 2024 kujitolea kumsamehe Trump ikiwa atachaguliwa tena White House.
Aliyekuwa Gavana wa Arkansas, Asa Hutchinson, mgombea urais wa chama cha Republican ambaye mara kwa mara amekuwa akimkosoa Trump, alilalamika katika mahojiano ya CNN kwamba wagombea hawakuzungumzia masuala bali Trump na changamoto zake za kisheria.