Rashid Ally Juma aka Chid Designer mzaliwa wa Tanga mwenye elimu ya Darasa la sita ambae leo hii amefanya makubwa kwenye Sekta ya Ushonaji nchini Tanzania.
Mbali na kwamba aliishia darasa la sita kutokana na changamoto za kifamilia aliamua kujikita ama kujihusisha na katika biashara nne ikiwemo hii ambayo imempa umaarufu nchini.
‘Ndio Maisha ya mtanzania lazima upitie kwenye magumu hivyo mimi kuishia kwangu Darasa la sita sio kwamba ndio nimefeli kimaisha hapana bali nimefanya vitu sana sana yaani nimejaribu biashara tofauti tofauti nilishatengeneza kucha wadada, nilishawahi kuwa fundi magari, nilishawahi kuuwa fundi kinyozi, vyote nilijaribu lakini sikufanikiwa na hatimae Mungu akaja kuniheshimisha kwenye biashara ya Ushonaji’– Chid Designer
‘Nakumbuka niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja ni mtu mkubwa tu ningependa kumtaja kwamba wacha nijaribu kwenye ushonaji huenda Mungu kaniandika huku na hatimae leo imenipa heshima na nimetoa ajira kwa vijana wenzangu wasiopungua 25’– Chid Designer
Mwanzo nilianza na Mashine mbili za ushonaji siku zote kwenye biashara lazima uanze na kidogo na unajua kadri biashara inavyozidi kuwa kubwa ndipo uhitaji wa watu unazidi kuhitajika kwahiyo pale ofisini kwangu Suti Bega nina vijana kwa sasa kuanzia mapokezi pia kuna vijana maalamu wao kazi yao ni kuwafuata wateja namna ya kuwathamini tunawafuata maofsini mwao na kuchukua vipimo’ vya suti, hivyo ni hatua kubwa nimepiga’– Chid Designer
‘Na Mafanikio haya haya ya Suti bega yameletwa na watu mbalimbali nisiseme uongo kila mmoja ana mchango wake kuanzia wanaoshona suti za Maharusi, Wasanii, Viongozi na hata Uongozi wa Young Africans wamekuwa wakinipa tenda ya kuwavalisha wachezaji wao hata uongozi mzima hii ni kubwa sana sikuwahi kuja kufikiria kama ningepata hii nafasi’ – Chid Designer
‘Sasa mbali na mafanikio hayo pesa inaingia lakini kuna usemi mmoja unasema unachokula wewe gawana na wenzako wanaokufanya wewe kuendelea kuheshimika mjini hivyo leo hii June 14, 2023 nimewakabidhi Pikipiki mafundi wangu wawili ni kama zawadi yangu kwao’– Chid Designer
‘Sina kikubwa ama mimi nina mahela hapana ila ninachojaaliwa na Mwenyezi Mungu basi ninahakikisha tunasaidiana kwa kidogo kinachoingia mfukoni mwangu, hivyo Wa kulia ndio nilianza nae miaka nane nyuma halafu wa kushoto ndio fundi ambae alikuwa mshauri kwenye masuala ya ushonaji’- Chid Designer
‘Mipango yangu kuja kutoa fursa kwa vijana hususani wa kitanzania kufungua Shule ya ushonaji unajua kuna najua kuna watu wanaichukua poa hii biashara lakini hii biashara asikuambie mtu ni biashara nzuri sana kama wewe ni kijana wa kitanzania unanisikiliza leo hii basi naomba pambania katika kile unachohisi kitaweza kukusaidia’- Chid Designer
‘Ukiacha na mpango niliousema kwasasa nina Brand mbalimbali ya viatu vyangu, Peni vyote vinapatikana Suti bega na Ofisi yetu inapatikana Dar es Salaam Sinza Maduka Vatican ama unaweza kuwasiliana nasi kupitia 📞 062 934 3534/📞WhatsApp 0714895465.’– Chid Designer
‘Kukaribia kwako wewe mtanzania kutatupa nguvu ya kuendelea kupambana na kujituma hakika Suti bega ni ya watanzania Vaa pendeza ni wakati wako sasa wewe kijana wa kitanzania na bei zetu ni za nafuu kuanzia Suti hata chochote unachohitaji sisi tunashona na mafundi wakisasa wenye ujuzi wa kushona nguo zote’- Chid Designer
“Mwisho ningemaliza kumshukuru Mke wangu kwani bila yeye kunivumilia hata kunipa Ushauri kiukweli nimeamini hakuna Mafanikio pasipo nguvu ya Mwanamke kwani amekuwa na mchango mkubwa pia pale ninapohitaji wazo fulani kipi niboreshe ama kipi nisikifanye juu ya biashara yangu anakuwa mstari wa mbele asante Msukuma wangu’- Chid Designer
Hapa akatuonesha baadhi ya picha ambazo ameshatoa huduma kwa mastaa na viongozi mbalimbali katika huduma yake ya Ushonaji.