Kila mwaka nchi mbalimbali duniani huadhimisha Siku ya Wachangia Damu Duniani (WBDD) ambapo tukio hili linasaidia kuongeza ufahamu wa haja ya damu salama na bidhaa za damu na kuwashukuru wafadhili wa damu wa hiari, wasiolipwa kwa zawadi zao za kuokoa maisha.
Na Maadhimisho haya maalum ni kuenzi umuhimu wa Elimu ya Uchangiaji wa damu ambapo kitafaita yamefanyika Mkoani Dodoma.
Hapa nimekuletea kile achokiandika Rais wa Young Africans, Hersi Said kupitia ukurasa wa instagram baada ya kupewa tuzo ya Yanga SC katika maadhimisho hayo ikiwa kama sehemu ya kutambua mchango wao katika Wizara ya Afya.
‘Leo hapa Dodoma, klabu ya Yanga SC imepata heshima ya kukabidhiwa TUZO MAALUM ya kuwa taasisi inayotambulika rasmi na wizara ya Afya katika uchangiaji wa damu’- Hersi Said Rais wa Yanga SC
‘Imekuwa ni desturi ya klab hii ya wananchi kuchangia damu kupitia kwa wanachama na mashabiki zake kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wenzetu wenye mahitaji kama wazazi, wagonjwa waliopata ajali na kadhalika’- Hersi Said Rais wa Yanga SC
‘Ama hakika TUZO hii ni heshima kubwa kwangu binafsi, ni heshima kubwa kwa klab yangu ninayo iongoza na ni heshima kubwa kwa wanachama na mashabiki wa klab hii bora kabisa nchini Tanzania na Afrika’- Hersi Said, Rais wa Yanga SC
Shukrani za dhati ziwaendee Wizara ya Afya chini ya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Taasisi ya ya Damu Salama Tanzania.