Kelly Clarkson alisema anashangazwa na watoto wake kwani bado wana ndoto ya yeye kurudiana na mume wake wa zamani Brandon Blackstock hata baada ya miaka mitatu ya kutengana kwao.
“Wakati wowote anapotajwa labda kuwa na mtu mwingine wanakataa kabisa wanaamini kuwa tungeweza kuwa pamoja na hatuko karibu kwa muda mrefu,” mwimbaji huyo aliiambia Glennon Doyle kwenye podikasti yake, ” Tunaweza Kufanya Mambo Magumu,” .
“Anytime there’s mention of him maybe being with somebody else they are just really adamant about keeping that dream alive that we might still be together — and we are never around each other,” “We Can do Hard Things,”
Clarkson alisema ni vigumu iwapo utaamua kubaki katika uhusiano usiokupa furaha wakati mwingine.
Lakini wakati alipomaliza na kukata uhusiano wake na baba wa watoto wake ilikuwa ngumu, alisema,
“Mimi ni mama bora, kama, baada ya [talaka]. Mimi ni mama bora zaidi kwa sababu nadhani unapokuwa mwaminifu kwako mwenyewe. , unaweza kuwa mwaminifu kwa wengine.Lakini wakati mwingine hujui kuwa unajidanganya.
“Mapenzi ni magumu. yanakushawishi sana kwamba unafanya jambo sahihi. Ni jambo gumu sana unapompenda mtu kwa undani nakuhisi ni jibu sahihi.”
Clarkson na mtayarishaji Brandon Blackstock walifunga ndoa mwaka wa 2013, na akawasilisha kesi ya talaka mwaka wa 2020 na wamebahatika kupata watoto wawili – River Rose, 8, na Remy, 7.
Licha ya talaka yake, Clarkson alifichua kuwa bado anaamini watu wanaweza kubadilika na hapendi kukata tamaa kwa watu.
Alisema hayo alijifunza na kuyaweka ndani yake na imani yake alipokuwa mdogo baada ya mchungaji kuwa kama baba kwake wakati hakuwa na baba.