Katika tukio la kushangaza, Tiktoker mmoja wa Ubelgiji aliandaa tukio la kuonekana amekufa na kisha kufika kwenye mazishi yake mwenyewe yaliyo andaliwa na familia yake kwa helikopta kwa alichodai kuwa alitaka kutoa somo kwa familia yake.
Kulingana na gazeti la The Independent, David Baerten, anayejulikana kwenye TikTok kama Ragnar le Fou, anasema alihisi ‘kutothaminiwa’ na jamaa zake, ndiyo maana alidanganya kifo chake na alifanya mzaha huo wa ili kuwafunza familia yake somo kuhusu umuhimu wa kuwasiliana.
Chombo cha habari kiliripoti zaidi kuwa video hiyo ilionyesha kuwa David mwenye umri wa miaka 45 alifika kwenye mazishi yake mwenyewe, huku waombolezaji wakitazama jinsi helikopta hiyo ikitua shambani na mlango kufunguliwa na kumuona nakuanza kukimbia kisha inakata na kuonesha watu wanaomzunguka , huku wengine wakinekana kuendelea kusogea eneo hilo alilokuwemo ili kumkumbatia na kumsalimia huku kikundi cha filamu kikirekodi tukio hilo.
Gazeti la Times la Uingereza liliripoti kwamba mmoja wa binti zake alisaidia kuanzisha jumbe za maombolezo kwenye programu kuhusu “kufariki” kwa babake.
“Pumzika kwa amani, baba. Sitaacha kuwaza juu yako,” aliandika. “Kwanini maisha hayana haki? Kwanini wewe? Ungekuwa babu, na bado ulikuwa na kila kitu chako.
Marafiki na wanafamilia wengi waliovalia mavazi meusi walihudhuria mazishi hayo ya uwongo labla yaaliyedai kufa kuonekana ndani ya helikopta hiyo akiwa hai.