Baadhi ya watu wenye ulemavu wapatao 10 wanaoishi katika mazingira Magumu wilayani Geita Mkoani Geita wamepewa Msaada wa pikipiki za mataili matatu (Bajaji) ili kuwapunguzia adha ambazo wamekuwa wakikumbana nazo katika shughuli za kila siku.
Msaada wa bajaji hizo umefadhiliwa na Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya kuiwezesha jamii inayozunguka maeneo ya mgodi huo.
Akikabidhi bajaji hizo kumi Zenye thamani ya Shilingi Milioni 100 kwa walengwa, Mkuu wa wilaya ya Geita Mh.Cornel Magembe amewataka wanufaika kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani pindi watakapoanza kutumia bajaji hizo huku akiwataka kuwa wangalifu zisiharibike.
Magembe ameshukuru Mgodi wa GGML kwa kuliona hilo katika kuisaidia Jamii ya Mkoa wa Geita kwani wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt ,Samia Suluhu Hassan kwa kuwathamini watu wake.
Mmoja wa wanufaika na Bajaji hizo Felix John ameishukuru GGML kwa Msaada huo pamoja na serikali ya Rais Samia Suluhu kwa kutambua Mchango wa watu wenye ulemavu ndani ya wilaya na Mkoa wa Geita .
Naye Meneja Mwandamizi wa Mgodi, Gilbert Mworia amesema Mgodi utaendelea kusaidia makundi yote kwa nafasi inayopatikan na hivo wameanza na walemavu 10 kila mmoja kupatiwa bajaji.
Magenge Hassani ni miongoni mwa walemavu 10 waliopata msaada huo wa bajaji kutoka Mgodi wa madini GGML ameishukuru kampuni hiyo na kuahidi kwenda kuitumia kwa ajili ya kujiinua kiuchumi kwenye familia yake.