Inawezekana ukawa mmiliki wa magari aina ya Ford ambay ni miongoni mwa kampuni kubwa za kutengeza magari nchini Marekani kwa sasa imeagiza magari milioni 1.4 yarejeshwe kutokana na hitilafu
Hitilafu iliyotajwa ni ya usukani ambapo takriban magari milioni 1.1 yaliyoundwa kwa mtindo wa kispoti yaliyokuwa yameuzwa Marekani Kaskazini yametakiwa kurejeshwa.
Magari mengine 200,000 yenye muundo wa Taurus yaliyoundwa kati ya mwaka wa 2010 na 2014 yanaweza kukutwa ana tatizo la kushika kutu kwa harakakwa matukio hayo yaliyofanywa hivi karibuni huenda yakaifanya kampuni hiyo kuvunja rekodi ya kutaka magari mengi zaidi yarejeshwe katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kurejeshwa huko kwa magari hayo kumetokea wakati sakata ya usalama inawakumba wapinzani wakuu wa kampuni ya hiyo ambao ni General Motors (GM).
GM iliwahi kulaumiwa kwa kutotoa ilani za kiusalama kwamba baadhi ya magari yake hata baada ya kubaini kuwa magari hayo yanazima ghafla,dosari hiyo imehusishwa na vifo 13,ingawa wasanifu wa Marekani wanaamini kuwa idadi hiyo itaongezeka.