Brazil ilicheza wakiwa wamevalia jezi za rangi nyeusi katika kipindi cha kwanza cha ushindi wao wa bao 4-1 dhidi ya Guinea nchini Uhispania kama sehemu ya kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi kwenye uwanja wa Espanyol huko Barcelona.
Hii inafuatia tukio la fowadi wa Brazil Vinicius Jr kufanyiwa vitendo na ishara za ubaguzi wa rangi mara kadhaa nchini Uhispania alipokuwa akiichezea Real Madrid katika kampeni zilizopita.
Vinicius alifunga penalti ya dakika za mwisho na kukamilisha ushindi wa kawaida kwa timu yake.
Mapema mwezi huu,wanaume saba waliadhibiwa kwa vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya Mbrazil huyo.