Bibi mwenye umri wa miaka zaidi ya 84 Lemi john mkazi wa kata ya kinunga wilayani Igunga mkoani Tabora ameuomba Rais wa Tanzania amsaidie kuingilia kati mgogoro wa shamba lake ambalo lilipatikana madini ya dhahabu baada ya kuwepo kwa mchimbaji anayedaiwa kuingia kwenye shamba lake lenye madini nakutaka kumuondoa licha ya kuwepo kwa zuio la kusimamishwa kwa shuguli za uchimbaji katika eneo hilo
Bibi huyo ambaye hawezi kuzungumza kiswahili amesema eneo lenye ukubwa wa hekari sita aliachiwa na mume wake lakini kutokana na kuwa maskini wanataka kumpora eneo lake
Afisa madini Mkoa wa Tabora Abel Madaha amesema kuwa ofisi yake imetoa leseni ya uchimbaji wa madini katika shamba hilo baada ya kukidhi vigezo
Mchimbaji huyo Mohamed Omary Mmari amesema hakuna zuio la uchimbaji wa madini lililotolewa