Mamlaka za Saudia zimewakamata watu kadhaa kote nchini humo kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya katika siku za hivi karibuni huku siku ya Jumapili, walinzi wa mpakani wa doria katika eneo la Al-Ardah la Jazan walizuia jaribio la kusafirisha kilo 90 za mirungi kisha doria za ardhini zikazuia jaribio la kusafirisha kilo 400 za mirungi, katika operesheni ya pili.
Aidha, mamlaka hiyo iliwakamata wananchi wawili kwa kujaribu kuuza kilo 151 za mirungi iliyokutwa ikiwa imefichwa kwenye gari lao.
Katika operesheni tofauti, mamlaka kuu ya Kudhibiti madawa ya kulevya iliwakamata wakaazi wawili wa Pakistani katika mkoa wa Jeddah kwa kujaribu kuuza kilo 9.5 za methamphetamine huku maafisa wa polisi katika eneo la Makka waliwakamata raia wawili wa Ethiopia wakijaribu kuuza kilo 2 za hashish.
Katika mkoa wa Rafha, polisi walimkamata mkazi mmoja wa kabila lililohamishwa kwa kujaribu kuuza kilo 18 za hashishi iliyokutwa imefichwa kwenye gari lake.
Taratibu za awali za kisheria zimekamilika na mihadarati yote iliyokamatwa imekabidhiwa kwa mamlaka na wale wote waliokamatwa wamepelekwa kwenye Mashtaka ya Umma.