Timu ya Wataalamu wa msaada wa kisheria kutoka Mama Samia Legal Aid Campaign ikishirikiana na RC wa Shinyanga, Christina Mndeme na Jeshi la Polisi Shinyanga wamefanikiwa kuzuia ndoa ya Binti aliyefaulu kuingia kidato cha tano lakini Wazazi wake waliamua kumuozesha katika kijiji cha Mwawaza nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga.
Timu hiyo ilifika eneo la tukio na kushuhudia zoezi la uzuiaji na kukamata walengwa ambapo RC wa Shinyanga amesema ndoa hiyo ililenga kuzima ndoto za Binti huyo.
Mndeme amesema Mkoa wa Shinyanga hauko tayari kuona Watoto wa kike wanashindwa kufikia ndoto zao kwa ajili ya Wazazi wachache wenye tamaa ya mali, ambapo ameagiza Wazazi hao ambao wametoweka kufika Kituo Kikuu cha Polisi Mjini Shinyanga…“Serikali ya Mkoa wa Shinyanga itasimamia Binti huyu apate haki ya msingi ya kupata elimu ili aweze kufikia ndoto zake”