Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ameongoza maombi mjini Vatican kwa ajili ya waathiriwa wa shambulio la kigaidi kwenye shule mmoja nchini Uganda.
Takriban watu 40 wengi wao wakiwa wanafunzi walishambuliwa kwa kupigwa risasi na kuchomwa moto hadi kufa katika mji wa Mpondwe, magharibi mwa nchi hiyo siku ya Ijumaa usiku, jeshi la Uganda limesema kuwa linawasaka wanamgambo hao kutoka kundi linalojulikana kwa jina la ADF.
Waliwateka nyara wanafunzi sita kabla ya kutoroka kuvuka mpaka na kuingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baada ya kutekeleza mauaji hayo, waasi hao wanaoendeleza shughuli zao mashariki mwa DRC, wametuhumiwa kwa kuwateka wanafunzi sita kabla ya kuvuka mpaka na kuingia nchini DR Congo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amelaani shambulio hilo ambalo amelitaja kuwa la kioga.
Kwa mujibu wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ameagiza kutumwa kwa wanajeshi zaidi katika mpaka wa nchi hiyo na DRC, baada ya shambulio la hilo.