Mzozo ulizuka katika mji wa Daegu nchini Korea Kusini siku ya Jumamosi huku maafisa wa eneo hilo wakiongozwa na meya wakipambana na polisi wakati wa maandamano ya kupinga tamasha la LGBTQ.
Wapinzani wakiwemo mashirika ya Kikristo walikuwa wametuma maombi ya zuio la muda dhidi ya Tamasha la Utamaduni la Daegu Queer, ambalo lilikuwa limepokea kibali cha polisi kufanyika na kudai kwamba hafla hiyo inaweza “kuchochea tamaduni mbaya ya ngono kwa vijana.”
Tukio hilo la kila mwaka lililofanyika kwa mara ya kwanza mnamo 2009 – liliruhusiwa kuendelea, na kusababisha Hong na wakosoaji wengine kubishana na kuleta usumbufu ambapo polisi walikuwa wameonya wiki iliyopita kwamba eneo hilo lingeshuhudia msongamano mkubwa kutokana na maandamano hayo, na kwamba litapeleka wafanyakazi kusaidia kudhibiti trafiki.
Mvutano uliibuka siku ya Jumamosi wakati maafisa wa serikali ya mtaa walipokusanyika kuandamana katika eneo la tamasha. Video iliyotumwa na waandaaji wa hafla hiyo inaonyesha magari ya tamasha yakiwa yamekwama barabarani, yakishindwa kuingia kutokana na waandamanaji.
Picha zinaonyesha idadi kubwa ya polisi wakifika kuwatawanya waandamanaji, wakisukuma umati wa watu wakiwa na ngao na mikono iliyofungamana ili kuunda kizuizi cha kibinadamu.
Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap lilikadiria kuwa takriban waandamanaji 500 na maafisa wa polisi 1,500 walikuwa kwenye eneo la tukio. Tamasha hatimaye liliendelea, gwaride likifanyika kama ilivyopangwa.
Hong, meya wa Daegu, aliwahi kugonga vichwa vya habari kwa kauli dhidi ya LGBTQ, kama vile kudai kwamba wanaume wapenzi wa jinsia moja wangedhoofisha jeshi la Korea Kusini, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.
Korea Kusini haitambui ndoa za jinsia moja kisheria, na haikubali wapenzi wa jinsia moja ikilinganishwa na demokrasia za karibu kama vile Japan na Taiwan.