Ukienda Marekani utaambiwa HAIER iliingia rasmi tangu mwaka 1999, Indonesia utaambiwa HAIER waliingia rasmi tangu mwaka 1996, pale Philippines ni tangu mwaka 1997, India ni tangu 2004…. hapo sijazitaja Nchi za Ulaya kama Ujerumani ambako Brand ya HAIER tayari ipo….. Tanzania tumechelewa kuletewa rasmi brand hii lakini hakijaharibika kitu, mwendo ndio kwanza tumeuanza na tena tumeuanza vizuri kwa sababu GSM inasimamia kila kitu.
Hatimaye GSM Group na HAIER wamezindua rasmi upatikanaji wa brand hiyo hapa Nchini Tanzania na kuiweka Nchi hii kwenye orodha ya Nchi za Afrika zinazofaidi teknolojia hii ya kisasa zikiwemo South Africa, Tunisia, Nigeria, Egypt na Algeria ( kwa uchache).
Kampuni ya HAIER ambayo ilianzishwa China miaka 39 iliyopita (1984) ni Kampuni bora ya utengenezaji wa bidhaa za kielektroniki kama vile friji, AC, TV, mashine za kufua n.k ambapo imefanikiwa kukuza mtandao wao wa rejareja na sasa zinapatikana kwenye Nchi zaidi ya 200 na kushinda Tuzo za ubora kwa miaka 14 mfululizo.
Tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa GSM na HAIER, tayari Wasambazaii na Mawakala wameshaanza kuziuza bidhaa hizi Nchi nzima lakini pia zinapatikana kwenye Maduka mawili makubwa yaliyozinduliwa Jijini Dar es salaam ambapo Duka kuu lipo Salamander Tower, Samora Avenue (Posta) na duka la pili lipo Uhuru Heights (Kariakoo).