Washukiwa 20 wamekamatwa kwa kuwa washirika wa ADF,”Allied Democratic Forces (ADF) yenye makao yake nchini DRC msemaji wa polisi Fred Enanga aliuambia mkutano na waandishi wa habari, akimaanisha
Alisema katika taarifa yake tofauti waliokamatwa ni pamoja na Mwalimu Mkuu na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Lhubiriha iliyopo Mpondwe, Magharibi mwa Uganda, ambao walishambuliwa Ijumaa jioni.
Enanga alisema kwa sasa waliofariki ni 42 wakiwemo wanafunzi 37,mkubwa zaidi kati ya wahasiriwa waliotambuliwa kufikia sasa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 95 na mdogo wa kike mwenye umri wa miaka 12.
Watu wengine sita walijeruhiwa na kubaki hospitalini, alisema huku akiongeza kuwa kuna taarifa zinazokinzana kuhusu idadi ya waliotekwa na wauaji hao kati ya watano hadi saba.
“Shambulio dhidi ya watoto wasio na hatia ni la kinyama, ni la kinyama na bila shaka ni uhalifu dhidi ya ubinadamu,” Enanga alisema.
Imebainika kuwa kwenye tukio watu hao walikatwakatwa kwa mapanga, kupigwa risasi na kuchomwa moto hadi kufa katika mabweni yao katika mauaji ya kutisha ambayo yamelaaniwa kimataifa.
Lilikuwa shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Uganda tangu milipuko miwili ya mabomu mjini Kampala mwaka 2010 kuwaua watu 76 katika shambulio lililodaiwa na kundi la Al-Shabaab lenye makao yake nchini Somalia.
Kundi la ADF, kundi lenye silaha ambalo kihistoria linahusishwa na waasi wengi wa Kiislamu kutoka Uganda wanaompinga Museveni, limekuwa likilaumiwa kwa maelfu ya vifo vya raia nchini DRC tangu miaka ya 1990.
Msemaji wa Polisi ya Uganda amesema, wao kama nchi wanaendelea kushirikiana bega kwa bega katika vita dhidi ya ugaidi.