Rais William Ruto amsema kuwa serikali itaongeza idadi ya watoto wanaonufaika na Mpango wa Kulisha Watoto Shuleni kutoka 1.6 hadi milioni 4.
Wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kulisha Shule za Kaunti ya Nairobi ,katika Shule ya Msingi ya Roysambu mnamo Jumanne, Juni 20, 2023, Ruto alisema kuwa serikali itaongeza bajeti ya mpango huo wa lishe kutoka Ksh5 bilioni hadi Ksh6 bilioni ili kupanua kundi la walengwa.
Katika hotuba yake, Ruto alieleza kuwa serikali itawasilisha bungeni bajeti ya ziada ya Ksh1 bilioni, ili kuendana na gharama inayotarajiwa kuongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watoto waliowekwa kunufaika na mpango huo.
Tazama hapa;