Takriban watu 31 waliuawa na saba kujeruhiwa wakati gesi ya kupikia ilipolipuka kwenye mgahawa mmoja huko Yinchuan kaskazini magharibi mwa China na kutajwa kuwa ajali mbaya zaidi kwenye historia ndefu ya China za viwandani, ambazo hutokea mara kwa mara licha ya ahadi za serikali za kubana viwango vya ufisadi na uangalizi duni unaolaumiwa mara kwa mara wa kuporomoka kwa majengo, mapango ya migodi, milipuko na majanga mengine. .Shirika rasmi la Habari la Xinhua limeripoti leo Alhamisi.
Shimo la kuchimba mgodi liliporomoka mwezi Februari katika eneo la Inner Mongolia ya kaskazini mwa China, na kuzika makumi ya watu chini ya vifusi na kuua 53. Kampuni inayoendesha mgodi huo ilitozwa faini mwaka uliopita kwa ukiukaji mwingi wa usalama.
Mlipuko mkubwa katika kiwanda cha kemikali kaskazini mashariki mwa Uchina uliua takriban watu 13 mnamo Januari watu wengine 35 walijeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea viunga vya mji wa Panjin mashariki mwa mji mkuu, Beijing.
Mlipuko huo ulitokea mwendo wa mbili na dakika arobani usiku saa za China sawa na saa tano na dakika arobani saa za Afrika ya Mashariki,katika Mkahawa wa Fuyang Barbecue, ulioko katika eneo la makazi katikati mwa jiji la Yinchuan, mji mkuu wa Mkoa unaojitawala wa Ningxia.