Kodak Black alidaiwa kukosa kipimo cha dawa kilichohitajika katika kesi yake inayoendelea ya jinai, na sasa anakabiliwa na shtaka lingine la uhalifu kwa sababu ya tukio hilo.
Kulingana na ripoti kutoka Local 10 Alhamisi ya juni 22, kibali kilitolewa cha kukamatwa kwa rapa huyo kisha mnamo Juni 14 baada ya kudaiwa kutojitokeza kwenye majaribio ya dawa za kulevya siku zilizopita na hii inakuwa ni mara ya pili kwa kukosa kipimo cha dawa kinachohitajika katika kesi inayoendelea na anatarajiwa kufika mahakamani kwa ajili ya kesi hiyo Jumatatu (Juni 26).
Awali Kodak Black alikamatwa mnamo Julai 16 mwaka jana kwa tuhuma za kusafirisha oxycodone pamoja na kuendesha gari na leseni na vitambulisho vilivyoisha muda wake,aliachiliwa siku iliyofuata kwa bondi ya $75,000 chini ya masharti madhubuti ya kuachiliwa kabla ya kesi ya kuwasilisha vipimo vya dawa wakati kesi inasubiri.
Kodak na timu yake ya wanasheria walifika katika chumba cha mahakama huko Broward mara baada ya kueleza kilichotokea.
Kulingana na wakili wa rapper huyo alikuwa nje ya mji alipotakiwa kufanya vipimo vya kwanza, na hata alisema vipimo vya mara ya pili aliofanya ilikuwa imechanganywa.
“There’s just so much with this that’s unjust and not right about this situation,” Kodak Black alisema wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
“Sio tu kwamba ninakanusha, lakini pia ninaumia kwa sababu tabia yangu inabatilishwa kwenye kweli na siwezi kuzungumza juu ya yote hayo kwa sababu sitaki kuifanya hadithi kuwa kubwa kuliko ilivyo … , mambo yote mazuri ninayofanya hayaonekani kamwe na sijui kwa nini.”